Posts

146 - Twae Wangu Uzima

146 - Twae Wangu Uzima "Take My Life" 1. Twae wangu uzima, Sadaka ya daima; Twae saa na usiku, Zikutukuze huku. 2. Twae mikono nayo, Ifanye upendavyo, Twae yangu miguu, Kwa wongozi wako tu. 3. Twae sauti yangu, Niimbe kwa Mungu tu; Itwae na midomo, Ijae neno lako. 4. Twae dhahabu pia, Na yote ya dunia; Twae yangu hekima, Upendavyo tumia. 5. Nia itwae, Mungu, Haitakuwa yangu; Twae moyo; ni wako, Uwezo makazi yako. 6. Twae mapenzi yangu, Sifa za moyo wangu; Twae kabisa nafsi, Niwe wako halisi (Amina)

147 - Uishi Ndani Yangu

  147 - Uishi Ndani Yangu "Live Out Thy Life Within Me" 1. Tawala ndani yangu, Ee Yesu, Mfalme.  Uwe kwangu majibu Kwa maswala yangu; Uishi ndani yangu, Wewe, mwongozi Utumishi ni wangu, Wako utukufu. 2. Hekalu nimetoa, Umelisafisha; Sasa fahari yako Imulike ndani; Dunia iwe kimya, Mwili sasa uwe  Mtumwa mtulivu Wa kukutii tu.  3. Viungo vyake mwili, Vyote vikungoja  Tayari vikiitwa Kwenda, kusimama;  Bila manung`uniko Au malaumu,  Au kusumbuliwa, Pasipo majuto. 4. Niwe na utulivu Pasipo haraka;  Tayari kungojea Maagizo yake.  Tawala ndani yangu. Ee Yesu, Mfalme,  Uwe kwangu majibu Kwa maswali yote.  (Amina)

148 - Univute Karibu

  148 - Univute Karibu "Close To THee My Father Draw Me" 1. Univute karibu, Baba, Unikumbatie;  Unisongeze kifuani, Nataka pumziko.   Univute karibu (Vuta, univute karibu)    Kwa kamba za upendo, (Kwa kamba, kamba za upendo)    Univute (Kwa kamba za upendo, Univute karibu)   Karibu nawe. (Univute karibu) 2. Univute Mwokozi wangu, Na tusiachane;  Mikono yako juu yangu Leo niione. 3. Univute kwa Roho yako, Nifanane nawe;  Unioshe, unihuishe, Niwe safi, huru. (Amina)

149 - Kuwa Wake Yesu

149 - Kuwa Wake Yesu "Would You Live For Jesus" 1. Kuwa  wake Yesu, Je! Ni kusudi lako? Ungeenda naye njia nyembamba? Unataka aubebe mzigo wako? Awe Mwongozi wako. Uwezo wake unakutosha Na damu yake itakusafi; Kwa vile ukubali ni bora Afanye mapenzi yake nawe. 2. Unataka kuitika anapokwita? Kupata amani kwa kumpa vyote? Wataka uwezo usianguke kamwe? Awe Mwongozi wako. 3. Wataka raha katika ufalme wake? Ungeshinda kwa majaribu yote? Ungefanya kazi yake vizuri sana? Awe Mwongozi wako. (Amina)

150 - Hacha, Maneno Mabaya Yasitoke

 150 - Hacha, Maneno Mabaya Yasitoke "Angry Words Oh!, Let Them Never" 1. Hacha, maneno mabaya Yasitoke Kinywani  Moyo mwema uzuie Ndimi, zisichafuke "Nanyi pendeni", Asema Yesu,   (mpendane) (mpendane)   Kama mwanzo alivyotupenda: "Nanyi pendeni", Asema Yesu,   (mpendane) (mpendane) Wana, tiini amri hii. (amri heri hii).  2. Pendo ni mtakatifu; Urafiki: mzuri:  Visiharibike mara Kwa kunena vibaya. 3. Tusinene kwa hasira, Inazaa huzuni.  Pendo lako, ee Mwokozi, Inatosha tushinde. (Amina)

151 - Huniongoza Mwokozi

  151 - Huniongoza Mwokozi "He Leadeth Me" 1. Huniongoza Mwokozi, ndipo nami hufurahi,  Niendapo pote napo, ataniongoza papo. Kuongoza hunishika; kwa mkono wa hakika;  Nitaandamana naye Kristo aniongozaye. 2. Pengine ni mashakani nami pengine rahani;  Ni radhi, ijapo yote, yupo nami siku zote. 3. Mkono akinishika kamwe sitanung`unika;  Atakachoniletea ni tayari kupokea. 4. Nikiisha kazi chini sitakimbia mauti;  Kuishinda ni ya hakika nikiongozwa na Baba. (Amina)

152 - Karibu Na Wewe, Mungu Wangu

152 - Karibu Na Wewe, Mungu Wangu "Nearer My God To THee" 1. Karibu na wewe, Mungu wangu; Karibu zaidi, Bwana Wangu. Siku zote niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu. 2. Mimi nasafiri duniani, Pa kupumzika sipaoni, Nilalapo niwe karibu na wewe, Karibu zaidi, Mungu wangu. 3. Yote unipayo yanivuta; Pa kukaribia nitapata; Na nielekezwe karibu na wewe; Karibu zaidi, Mungu wangu. 4. Na kwa nguvu zangu nikusifu, Mwamba, uwe maji ya wokovu; Mashakani niwe, karibu na wewe, Karibu zaid, Mungu wangu. 5. Na nyumbani mwa juu, Baba yangu; Nikinyakuliwa toka huko, Kwa furaha niwe pamoja na wewe, Karibu zaidi Mungu wangu. (Amina)